SOMA HAPA ILI UWEZE KUMJUA MKE WAKO AU MUME WAKO SAHIHI NI YUPI.

leo nimeona nikuonyeshe tabia za watu wote katika mapenzi zikoje ili wewe mwenyewe uanze kujua ni mume au mke yupi unataka awe wako.ingawa makala ijayo ntafafanua zaidi nani anatakiwa amwoe nani lakini leo nimeona nitangulie kueleza tabia za watu wote katika mapenzi zikoje ili nawewe mwenyewe ujijue ukoje katika mapenzi.
Ntatumia jina lako kukuonyesha wewe ukoje katika mapenzi kwakuwa jina lako ndo wewe mwenyewe na wewe mwenyewe ndo jina lako.
Yani naamanisha jina lako lilivyo ndivyo ulivyo!,na biblia inasema 1Samweli 25:25 “Nakusihi, Bwana wangu, wewe usimwangalie huyu mtu asiyefaa, yaani, Nabali; KWA MAANA KAMA LILIVYO JINA LAKE NDIVYO ALIVYO YEYE; jina lake ndilo Nabali, na upumbavu anao; lakini mimi, mjakazi wako, sikuwaona hao vijana wa bwana wangu aliowatuma”
jina lako lina siri nyingi sana ndani yake,maana ndani yake linaelezea wewe ni nani,unapenda nini,unaweza nini,udhaifu wako,imani yako,karama yako,una sifa gani katika mapenzi n.k
Ndo maana waganga wakitaka kuroga huwa wanataka jina tu la mtu,kwakuwa wanajua wakilipata wamempata mhusika.
Katika mapenzi kila mmoja amekuwa na tabia ya aina fulani lakini tabia hizo zinatoka kwenye majina yao...
Kwa mwenye herufi A au M au Y.
Wenye herufi hizi ni wakali na wachangamfu, wenye hisia na wanaoweza kujieleza wakiwa na ari ya kufanya chochote. “SASA HIVI” hayo ndio mambo wanayotaka kusikia.
Ni watu wasiokuwa na subira, kila kitu kinafanyika kwa msukumo na haraka haraka. Ni viongozi majasiri ambao hawaoni karaha kuchukua majukumu, wakati wote wanajiona kwamba “Wanajua sana”.
Kwa ujumla wenye herufi hizi ni watu wenye mapenzi motomoto, tatizo lao kubwa hawapendi kusikiliza ushauri wa kimapenzi, na hawakubaliani na mambo nusu nusu. Ni watu wenye kutegemea mazuri wakati wote na hawakubali kushindwa. Hupenda kukimbilia katika mapenzi bila kufikiri, wanapohisi wamepata mpenzi wa kweli. Ni wepesi kuvutwa katika mapenzi na ni wenye miamko ya ghafla au misukumo ya kiwazimu ambayo wakati mwingine inawafanya waonekane wapumbavu.
Mwenye herufi B au N au Z
Wenye herufi hizi ni waaminifu sana katika mapenzi na wanaohitaji ulinzi katika mapenzi na njia au mwenendo unaoeleweka.
Pamoja na kwamba asili yao ni udongo,wanaweza kuwa ni wenye mahaba na mapenzi makubwa kwa wapenzi wao.
Uhakika wa mapenzi ndio jambo kubwa ambalo wenye nyota hii huangalia kwanza na baadae Penzi hilo liwe lenye hisia na mpangilio.
Pamoja na hisia kali walizonazo, wao ni watu imara na wasiobadilika hivyo kuwafanya watu wenye shauku kutovutiwa nao.
Uaminifu ni jambo la pili ambalo wenye nyota hii wanalo hivyo kuwafanya wao wawe watu wenye kuaminika na hiyo inasababisha wawe wenye wivu kupindukia.
Wanachotakiwa kufanya ni kujitahidi kuwapa nafasi wapenzi wao la sivyo watajikuta wako peke yao. Ndoa kwao ndio uamuzi mzuri kuliko kuishi na wapenzi. Tabia yao ni ya kudumisha jambo fulani wanaloliamini au walilolianzisha na hawapendi kubadilishwa.
3.Kwa wenye herufi C au O.
Watu wenye herufi hizi wanajulikana sana kwa hadhi yao ya kuwa na sura mbili. Kuna wakati wanakuwa na hisia tofauti na muda si muda wamebadilika.
Pamoja na kwamba hawapendi kubanwa sana , ni watu wachamgamfu na wenye mahaba mazuri.
Ni watu wenye asili ya mawasiliano na ni vigumu sana kuwafanya wajinga hivyo basi wakishampenda mtu wanahakikisha kwamba hawamchoshi huyo mpenzi. Watatumia muda mrefu kuzungumza maneno mazuri na wapenzi wao ili kuhakikisha kuwa uhusiano unazidi kuwepo.
Katika mapenzi, wao wanapenda vitu tofauti tofauti na wanahisi wamechoshwa basi huwa wa kwanza kuondoka aidha kwa muda au moja kwa moja.
Uaminifu ni kitu kigumu kwa watu wenye nyota hii na wanahisi kwamba kuna kitu wanakikosa nje hivyo basi wanatoka sana nje hata kama wakiwa wana ndoa yenye furaha.
Wengi wao wanafikia hatua ya kuishi maisha ya sehemu mbili; mke na bwana au bwana na mke.
Wenye herufi D au P.
Hisia ni kitu muhimu sana katika mapenzi kwa wenye herufi hizi, pamoja na kwamba kimaumbile ni watu wanapenda kujilinda na wanaogopa sana kuumizwa kimapenzi na wapenzi wao.
Wanapenda sana kuwa karibu na wanayempenda na kuwaonyesha huba na upendo mkubwa. Kwao hakuna mapenzi ya nusu nusu na wanapenda sana kuwa na mtu ambaye atadumu nae milele.
Wenye wenye herufi hizi bila ya kuwa na mpenzi hujihisi hawajatimiza lengo lao katika maisha hivyo basi huwa hawana raha.
Ni wapenzi waaminifu na wanategemea wapenzi nao wawe waaminifu kama wao.
Ni wagumu sana kuachana na wapenzi na inapotokea huwa hawaagi wako radhi wao waumie kuliko kuachana na anayempenda.
Wenye herufi E au Q
Tabia yao ni kujitanua, Ukarimu na ulezi ikichanganyika na ujeuri na kujionyesha, na hiyo huwaharibu wale wanao wapenda.
Furaha haina mpaka katika mapenzi yao, mioyo yao mikubwa na hisia zao nzito hutokeza dhahiri wanapompenda mtu.
Baada ya hapo ndipo sura yao kamili hujitokeza. Wao wanathamini sana mapenzi na juu ya jambo lolote, na wanaweza kuwa waaminifu sana na wakati mwingine huwaabudu wapenzi wao.
Wanapenda kujishughulisha sana na mambo ya mapenzi lakini mambo yakiharibika basi inakua vigumu sana kuyatengeneza.
Tatizo lao kubwa ni wao kujisahau kwamba ni upande mmoja wa penzi na wanajifanya wao ndio viongozi.
Kwa nje wanaonekana ni wenye kujiamini katika mapenzi lakini kwa ndani wanaweza kuwa wanaumia lakini hawawezi kukubali. Hata hivyo mara nyingi hutegemea kupata hisia kama walizonazo wao kutoka kwa wapenzi wao.
Wenye herufi F au R
Pamoja na kwamba wanaonekana ni watu wenye aibu kwa undani na kujiamini, wenye nyota hii hupumzika na kunawiri wanapokuwa katika mapenzi.
Ni watu ambao inawawia vigumu kuonyesha penzi lao. wana mtizamo wa kufikiri kabla ya kujitumbukiza ndani ya penzi lolote, wanachunguza kwa makini matokeo ya penzi lenyewe.
Wanapotafuta mpenzi wanaweza wakakupumbaza na maneno matamu na raha zisizo na kifani. Ni vizuri kufikiria mara mbili kabla hujajiingiza katika mapenzi na wao.
Inawawia vigumu wao kukuanza wewe kimapenzi kwa sababu wana uhakika kwamba watashindwa.
Kinachowasaidia ni subira na kuwaelewa wapenzi wao ndio maana mapenzi yanakua.
Mara wakishapata mpenzi wa kweli wanakuwa waaminifu sana na watafanya kila njia kuhakikisha mapenzi yanakuwa hai na yenye kupendeza.
Hata hivyo wanaweza kuwa wasumbufu, wenye kulalamika na wenye mtizamo wa makosa madogo madogo kwa mpenzi wake ili amshutumu.
Kwa sababu ya hali yao hii mara kwa mara kunakuwa na ugomvi wa wapenzi ambao wanataka kutekeleza malengo yao,pia hupenda kubembelezwa.
Wenye herufi G au S
Kujihusisha na suala la mapenzi kwa wenye herufi hizi ni kitu cha kawaida kabisa pamoja na kwamba wenye herufi hizi wanachukua muda mrefu kufanya maamuzi na inawawia vigumu sana kuchagua kati ya wapenzi wawili yupi anaefaa. Kwao kuishi vizuri ni kuwa na mpenzi au uhusiano wa kimapenzi.
Wenye herufi hizi wanathamini sana mapenzi kuliko hata maisha yao wenyewe na wanapenda sana kujionyesha kwamba wanapendwa.
Kwa sababu hizo wengi sana wanapumbazwa na mapenzi na ndoa zao zinakuwa zina matatizo na zisizo na raha kwa sababu ya kuoa mapema bila kuangalia. Wenye herufi hizi wanaonelea bora kuishi katika ndoa yenye matatizo kuliko kuishi peke yao.
Katika suala la mahaba (Romance) na ngono (Sex) wao ni mabingwa. Wanajua sana kumpendeza mwanamke au mwanaume kwa maneneo matamu yenye mpangilio na zawadi za thamani na wawapo kitandani wanatumia muda mrefu kuwachezea wapenzi wao sehemu nyeti.
Kwa ujumla wenye herufi hizi wanapenda kuishi vizuri na wanapenda wapenzi wao nao waishi katika hali nzuri.
Wenye herufi H au T
Watu wenye herufi hizi wanapenda sana kutumia fursa ya kufanya mapenzi kama njia mojawapo ya kuonyesha ujasiri wao katika mapenzi na namna wanavyojua kufanya tendo la ndoa.
Kwao mapenzi au tendo la ndoa ni kiungo muhimu sana katika maisha yao hasa ikizingatiwa kwamba nyota yao inatawala sehemu za siri. Inashauriwa wale wenye moyo mdogo wasifanye mapenzi na wenye herufi hizi la sivyo watajuta. Kitu kingine ni kwamba ni watu ambao hawayumbi na hawakubali kushindwa upesi.
Ni watu wenye ashki na hasira wakiwa wamedhalilishwa au wameumizwa na wapenzi wao na wanapofanya tendo la ndoa hasira zao huisha mara moja.
Ni watu wasiri sana katika masuala ya mapenzi na wanakuwa hivyo ili waweze kuwapata wapenzi wengi kukidhi matakwa au kiu yao kubwa ya ngono.
Mwenye herufi I au U.
Pamoja na kwamba wenye herufi hizi wanapenda wawe huru na wenye kujiamulia mambo yao wenyewe huwa wana starehe na kuona raha wanapokuwa ndani ya uhusiano wa kimapenzi.
Wenye herufi hizi wanapenda sana kujihusisha na makundi makundi lakini huwa wanapata muda wa kuwa na wapenzi wao. Ni watu wachangamfu na wenye kupenda lakini tabia yao ya kutojali inawafanya wapenzi wao wajione kwamba wanakosa ulinzi wa kimapenzi.
Wanapoingia katika mapenzi wanakuwa waaminifu. Mwanzoni wanakuwa wagumu sana kujihusisha. Wanapenda sana wakati wote kuwa na wapenzi wapya au mapenzi ya kawaida kwa sababu wanaamini mapenzi ya kudumu yanawanyima uhuru.
Wapenzi wao wanaponyesha dalili ya kuwapenda basi wao huwa wanajiondoa kwa hofu ya kubanwa na kutokuwa na uhuru.
Ni watu wanaopenda kufanya ngono kwa muda mrefu na hisia zao ziko mbali na inashauriwa kwamba wapenzi wao wawe wamekula kabla ya tendo la ndoa vinginevyo itakuwa taabu.
Mwenye herufi J au V
Watu wenye herufi hizi wanakuwa ni watu wenye aibu sana kwa wapenzi wao lakini aibu ikishawaondoka huwa ni wapenzi wa kutisha, kwa maana ya kwamba kwa vile wao ni waaminifu wanataka wapenzi wao wawaunge mkono katika hisia zao za kimapenzi.
Ni watu wanaoogopa sana kuachwa na wapenzi wao hivyo basi huwa wanakuwa waangalifu sana katika kuchagua wapenzi.
Jambo jingine ni kuwa huwa wao wenyewe hawajiamini kimapenzi, mara nyingi wanashindwa kuingia katika mapenzi kwa woga tu hivyo kukosa nafasi nzuri ya kupendwa.
Kwa ujumla ni wapenzi makini na huwa hawaoi wala kuolewa mpaka wapate uhakika wa kutosha kutoka kwa wapenzi wao. Ni wapenzi makini, waaminifu na wanaoweza kuaminiwa. Lengo lao katika mapenzi ni usalama.
Mwenye herufi K au W.
Wenye herufi hizi ni watu wanaopenda uhuru na hawawezi kabisa kukubali kudhibitwa katika mapenzi, mawazo yao na miono yao inaweza kubadilika mara moja na kuwa wakaidi na wasumbufu. Pamoja na kwamba ni waaminifu na wanatoa msaada mkubwa kwa wapenzi wao.
Wako tayari kutulia katika mapenzi iwapo watahakikishiwa uhuru wao na haki ya kutoingiliwa katika mambo binafsi. Niwa watu ambao hawapendi kuonyesha hisia zao halisi na wanachukua muda mrefu kuingia kikamilifu katika uhusiano wa kimapenzi.
Mara nyingi inakuwa vigumu kwao kuwaamini wapenzi wao lakini wakisha waamini wanakuwa waaminifu.
Ni watu wenye kusema mambo bila kuficha na mara nyingi hawaeleweki kwa wapenzi wao.
Katika ngono kwa sababu ya kupenda uhuru huwa wanapenda kufanya mambo wanavyotaka wao na hawakubali kuingiliwa au kufanya ngono mpaka watake wao na si wapenzi wao.
Wakati mwingine hushindwa kuelewa hisia za wapenzi wao jambo ambalo linawafanya wapenzi wao washindwe kuwaelewa.
Mwenye herufi L au X.
Wenye herufi hizi ni wenye kukamilika na Mahaba mengi na wanapenda sana kujitumbukiza na kuzama kwenye dimbwi la mapenzi.
Kuwa katika mapenzi ni kitu wanachokipenda na kukifurahia sana. Ni waangalifu wazuri kwa wapenzi wao wana huruma nyingi.
Ni watu wenye hisia kali za kimapenzi na ni wepesi kuathirika.
Mara nyingi huwa waoga wa vitu vya kimapenzi kwa sababu ya kuogopa kuvurugika kwa mipango yao ya baadaye.
Ni watu wenye kuyachukulia mapenzi kama ua la waridi na wanawaona wapenzi wao kama binaadamu wasio wa kawaida.
Tatizo lao kubwa la kimapenzi ni kwamba wanawaamini sana wapenzi wao na wanakuwa na mawazo au firika za kimapenzi ambazo hazipo katika dunia hii.
Kwa ujumla wenye herufi hizi wanapokuwa katika mapenzi wanakuwa wamejawa na shauku na mifano ya kuvutia na wanapenda wapenzi wao waishi kiroho. Mategemeo yao yanakuwa makubwa na yasipotimia huwa wanavunjika moyo.​.
****************"************
Kama mume au mpenzi wako uliye nae ana moja kati ya tabia ambazo nimezieleza hapo lakini hujazipenda,unaweza kupata msaada na ushauri wa kiroho kutoka kwangu,nipigie kwa namba hizi 0764694016

Comments

  1. Kweli nimeamini maana yanayotokea kwa huyu niliyenaye hata kwangu ni yenyewe haswaa yaliyoelezwa kutokana na jina langu na lakwake

    ReplyDelete
  2. Mmmh aiseee mbon mi nipo sawa Na mtu wangu

    ReplyDelete
  3. No kweli yanayonitokea kwenye Nyota y'all Jonathan LA herufi yang

    ReplyDelete
  4. Je kuna ewezekano mtu mwenye erufi F na V kuwa kwenye mausiano ya kudumu?

    ReplyDelete
  5. Je mwenye herufi T anapaswa kuwa kwenye mahusiano na mtu mwenye herufi C au R

    ReplyDelete
  6. Mwenye Jina helufi R anatakiwa kuwa na group gani ili waendane

    ReplyDelete
  7. Kwenye herfi s naweza kuwa na mtu kwenye herfi gan wakaowana nae

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni kweli kabisa mimi herufi ya mwanzo ya jina langu ni D na mpenzi wangu ni M lakini hatupatani hata kidogo kila siku ugomvi

      Delete
  8. Mwenye herufi Janaweza kuwa na mtu mwenye herufi gani kimapenzi

    ReplyDelete
  9. Mimi naitwa Hussein mpenz wangu anaitwa Aziza hivi tunaendana kweli nikija kumowa tafadhali nisaidie jibu

    ReplyDelete
  10. Na je f na f ni sawa kwenye mapenzi ama ndoa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yaan hili swali naomba sana lijibiwe kwa mwenyew F.. na F kweli wanaendana

      Delete
    2. Anaye jua majibu basi aweze kutujibu herufi hizi mbilii.... Wanaendana ambayo ni F... NA F...

      Delete
  11. Je mwenye herufi s anatakiwa awe na mwenye herufi gani apo.

    ReplyDelete
  12. G & L tunaweza dumu kwenye ndoa

    ReplyDelete
  13. Ni kweli maana kipimo ni mm mwenyewe

    ReplyDelete
  14. Kwa zaidi ya miaka 13 ya ndoa sikuweza kuzaa, naendelea kuharibika hata nikipata mimba, madaktari wote hawakuweza kunisaidia, hadi dada yangu akanielekeza kwa Dr DAWN, ambaye alinisaidia nikapata ujauzito na sasa hivi kuwa na mtoto mzuri wa kike,
    Anasaidia pia marafiki zangu wengi niliowaelekeza, Dr DAWN ni baraka kwa kila mtu anayewasiliana naye,
    *Kama unataka kupata mimba.
    *Ukitaka kuacha kuharibika kwa mimba.
    *Ukitaka kumrudisha mpenzi wako.
    *Kama unataka mume/mkeo arudishwe.
    *Kama unataka kurejesha mali yako iliyoibiwa au Pesa.
    *Ukitaka kutibu aina yoyote ya ugonjwa,
    Wasiliana naye kwa WhatsApp: +2349046229159

    ReplyDelete

Post a Comment