IJUE SIRI NZITO ILIYO JIFICHA KWAKO

Watu wengi husoma katika kitabu cha mwanzo 17:5-15 na kusema Mungu aliwabadilisha abrahamu na sarah majina yao,lakini si kweli Mungu hakuwabadilisha majina yao bali alienda kufanya marekebisho machache katika majina yao,namaanisha kwamba hawakupewa majina mapya bali yalifanyiwa marekebisho majina yao yaleyale waliyo kuwa nayo kwa kutoa herufi zilizo kuwa zimekaa mahali pasipo takiwa na kuziweka panapo takiwa ikiwa ni pamoja na kuziondoa kabisa zile ambazo zilikuwa hazihitajiki katika muundo wa majina yao.
Usisahau kuwa marekebisho hayo yalifanyika wakati anaenda kuwapa mtoto,hivyo inamaana kuwa muda wote walio kuwa wanateseka kuhusu mtoto tatizo lilikuwa kwenye hizo herufi zilizo kuwa zimekaa pasipo takiwa katika majina yao,
Kutoka Abramu ikawa Ibrahimu,
Na kutoka sarai ikawa sara.
Yatazame vizuri hayo majina na ujiulize yamebadishwaje?ni yaleyale ila kuna herufi I mwisho wa jina la sarai imeondolewa na kuwekwa mwanzo wa jina la abrahamu ili wapate mtoto(kwa abrahamu imeongezwa herufi H na I katikati ya jina).
Kama herufi i peke yake ilimpa sarai mateso yote hayo ya ugumba mpaka uzeeni mwake ilipo kuja kutolewa na Mungu ndipo akapata kicheko basi herufi za majina yetu si zakupuuzwa kabisa,kwakuwa zimebeba maana kubwa sana katika maisha yetu,huenda kuna herufi moja tu kwenye jina lako ndo iliyo zuia usipate kazi,elimu,mke au mume na kuweka mateso pasipo wewe mwenyewe kujua.
Unaweza kujua nyota yako (adress yako ya kiroho) kwa kupitia herufi ya mwanzo ya jina lako,
Katika ulimwengu wa mwili herufi moja haiwezi kuzungumza jambo moja kwa moja mpaka ziungane herufi zaidi ya moja ndipo zinaitwa neno na hilo neno lililoundwa na herufi linaweza kutoa maana au kuzungumza jambo.
Lakini katika ulimwengu wa roho herufi moja tu inaweza kuwa neno au maneno yenye maana ndefu sana kuliko maana ya maneno 10 ya kawaida.
Mfano katika biblia kitabu cha danieli 5:25 "na maandiko yaliyo andikwa ni haya MENE,MENE,TEKELI NA PERESI"
Tafusiri ya neno MENE tu likiwa peke yake ni hii "Mungu ameusahau ufalme wako na kuukomesha" unaweza kushangaa kwakuwa tafasiri ni ndefu kuliko neno lenyewe,ndo maana waliitwa waganga na wenye hekima wakashindwa kutoa tafusiri ya maneno hayo kwakuwa hawakuwa wanajua ndani ya neno MENE kila herufi katika mahali ilipo kaa ilikuwa ikizungumza jambo,kwahiyo anaetaka kujua tafasiri ya lile neno MENE anapaswa aanze kutafuta tafasiri ya herufi zilizopo kwenye lile neno kwanza kabla hajalitazama neno zima kwa ujumla,hapo tu ndo waganga na wenye hekima walipo kwama kwakuwa hawakwenda kutafuta maana ya herufi za yale maneno bali walikuwa wakitafuta maana ya yale maneno wakakuta ni maneno mapya kabisa wasiyo yajua tena hayapo kwenye lugha yoyote duniani.
Leo nataka nikuonyeshe herufi ya mwanzo tu ya jina lako imesababisha yapi ili usidharau herufi tena.
HERUFI A
Mwenye jina linaloanziana na herufi A ni mtu anayependa mambo makubwa, anajiamini na mwenye uwezo wa kutimiza malengo yake. Ni mtu mwenye tahadhari, mchangamfu na mpenda matukio. Anapenda Kuheshimiwa, anapenda Mamlaka, na ana kiburi, na hasira.
HERUFI B
wenye jina linaloanziana na herufi B ni mtu, mkarimu, muaminifu, na hupenda kazi. Ni Jasiri, shujaa na mkatili katika vita au pale anapotaka kulinda vilivyo katika himaya yake.
HERUFI C
Mwenye jina linaloanziana na herufi C ni mtu wa kukubadilika badilika, mshindani na hupenda kupigania malengo yao wanayopenda. Ni watu wa wabunifu na wanaopenda mawasiliano.
HERUFI D
Mwenye jina linaloanziana na herufi D ni mtu anayependa usawa, Biashara. Ni watu wanaopenda kuamrisha na mwenye kupenda usafi. Ni jeuri na wenye msimamo.
HERUFI E
Mwenye jina linaloanzia na herufi E ni mtu mwenye roho nzuri ,yenye mapenzi na huruma. mwenye kupenda uhuru katika mapenzi na mchangamfu. Kinyume na hivyo atakuwa ni mtu asiotegemewa na kigeugeu.
HERUFI F
Mwenye jina linaloanzia na herufi F ni mtu mwenye mapenzi,huruma , roho nzuri na ana uwezo wa kuwafariji watu. Ni mtetezi wa watu na mwenye huzuni lakini ni mzito wa kufanya maamuzi.
HERUFI G
mwenye jina linaloanzia na herufi G ni mtu mwenye mwenye imani ya kidini na nguvu za kiroho. Ana kipaji cha kubuni na uwezo wa kutatua matatizo ya watu. ni mtu mwenye hisia kali,msomi, mpweke na mkaidi wa kukubali ushauri wa kutoka kwa watu.
HERUFI H
Mwenye jina linaloanzia na herufi H ni mtu mwenye ubunifu na nguvu katika biashara, hupata faida kubwa kutokana na jitihada na bidii zake. ni mwenye mawazo mengi, mchoyo na mbinafsi.
HERUFI I
Mwenye jina linaloanzia na herufi I ni mtu mwenye kupenda sheria, ana huruma na utu. Wakati mwingi hajiamini na ni mwenye hasira za haraka.
HERUFI J
Mwenye jina linaloanzia na herufi J ni mtu mwenye matamanio,mkweli, mkarimu na muerevu. asiyekubali kushindwa na hupata mafanikio makubwa. Wakati mwingine anakuwa ni mtu mvivu na aliyekosa mwelekeo.
HERUFI K
Mwenye jina linaloanzia na herufi K ni mtu mwenye jeuri. mwenye msimamo thabiti,mashuhu
ri na mwenye uwezo wa kushawishi na kuamsha hisia za watu wana uwezo wa utambuzi ambao watu wengi hawana. ni mtu asioridhika na hali ya kimaisha.
HERUFI L
Mwenye jina linaloanzia na herufi L ni mtu wa vitendo, mwenye hisani na aliyejipanga vizuri kimaisha. Huwa wanapata ajali mara kwa mara.
HERUFI M
Mwenye jina linaloanzia na herufi M ni mtu mwenye kujiamini sana, mchapakazi na hupata mafanikio. ni mtu mropokaji,mwenye haraka na mwepesi kukasirika.
HERUFI N
Mwenye jina linaloanzia na herufi N ni mtu mwenye ubunifu, hisia kali na hupenda kuwasiliana lakini ana wivu sana.
HERUFI O
Mwenye jina linaloanzia na herufi O ni mtu mwenye subra, mvumilivu na mwenye bidii ya kusoma. Ni mtu mwenye kupenda kutumikia jamii na mwenye uwezo mkubwa wa kudhibiti hisia.
HERUFI P
Mwenye jina linaloanzia na herufi P ni mtu mwenye uwezo wa kuamrisha na hekima kubwa. Ana nguvu za kiroho lakini anapenda sana kujitumbukiza kwenye mambo ya watu.
HERUFI Q
Mwenye jina linaloanzia na herufi Q ni mtu mwenye kupenda mambo ya asili. Ni watu wasiyoelezeka nawana uwezo wa kuonyesha vitu visivyojulikana hata hivyo ni mtu aliyepooza sana.
HERUFI R
Mwenye jina linaloanzia na herufi R ni mtu mwenye uvumilivu, wenye huruma lakini ana hasira za haraka. Muda wote anakuwa mpenda amani.
HERUFI S
Mwenye jina linaloanzia na herufi S ni mtu mwenye mvuto mkali wa kuleta utajiri. Ni watu wenye maamuzi ya ghafla na hupenda mageuzi makubwa.
HERUFI T
Mwenye jina linaloanzia na herufi T ni mtu mwenye kupenda ushauri wa kiroho, anatumia nguvu za ziada kusaidia watu na hupata mafanikio baada ya muda mrefu. Ni watu wenye hisia kali sana na ni wepesi kushawishika.
HERUFI U
Mwenye jina linaloanzia na herufi U ni mtu mwenye bahati kubwa kwa ujumla. Anapenda uhuru katika mapenzi. Lakini ni mtu mbinafsi, mwenye tamaa na aliyekosa maamuzi.
HERUFI V
Mwenye jina linaloanzia na herufi V ni mtu Mchapakazi, wenye bidii na asie choka. Hata hivyo ni watu wasiotabirika.
HERUFI W
Mwenye jina linaloanzia na herufi W ni mtu muwazi, wachangamfuu kupita kiasi na mwenye uwezo wa kutambua mtu mwema na mbaya. Ni watu wenye tamaa na hufanya mambo ya hatari.
HERUFI X
Mwenye jina linaloanzia na herufi X ni mtu asiyependa kuwekewa vizuizi katika kwenye anasa na ni rahisi kujiingiza kwenye uzinzi na kujitoa uaminifu.
HERUFI Y
Mwenye jina linaloanzia na herufi Y ni mtu mwenye kupenda Uhuru na hawapendi kupingwa jambo lao lolote. Ni watu wanaokosa uamuzi na husababishia kupoteza bahati katika maisha.
HERUFI Z
Mwenye jina linaloanzia na herufi Z ni mtu mwenye kupenda matumaini na amani. Ni wenye msimamo mkali ila wanashauriwa kufikiria kabla ya kuamua jambo.
Mengi zaidi nitayaweka katika makala yangu itakayo fuata usikose.

Comments